Usalama Na Afya

Micshariki Africa & Adam Shule Kongwe


5:26
#1

 The easy, fast & fun way to learn how to sing: 30DaySinger.com

As long as unapewa chako unatembea/
Iwe mshahara au kifuta jasho unapokea/
Na kesho unarudi tena na kazi inaendelea/
Ndo unajikuta unafanya kazi kimazoea/
Cha msingi mkono uende kinywani/
(au sio) na watoto waende uani/
(namna hiyo) , muhimu unaingiza cash flani/na kazi ni halali wala haijalishi kazi gani/
Ndivyo ilivyo vivo hivyo hilo liko wazi man/
Ila jiulize kazi yako ina usalama kiasi gani/
Yaani! Mazingira ya kazi yakoje/
Ni salama au kuna hatari yoyote/
Sio  sababu haujawahi kudhurika/
Ndio iwe guarantee kuwa hupaswi kujiuliza/
Majuto ni mjukuu ni vizuri ukabadili/
Usiishie kuridhishwa na kauli ya mwajiri/
Yeah! Kauli ya tajiri au bosi/
Bila wewe kuchunguza mazingira haitoshi/
Hili swala ni la kufanyia kazi kwa pamoja/
Ni lazima kuzuia ajali na magonjwa/

Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini

Kwa kuwa bado mapema yani bado alfajiri/
Well.. Ngoja nianze na mwajiri/
Kama sheria peke yake inatosha unatuambia/
Mbona kuna watu wanakufa na kuumia/
Law pekee hazileti usalama kazini/
Ni wajibu kujilinda na kuwalinda wengine/
Toa mafunzo kwa miaka miwili mara moja/
Kila mtumishi ahudhurie bila kukosa/
(ili) aelimishwe anayofaa kutekeleza/
Iwe vifaa  au mashine anayofaa kuendesha/
Wape tahadhari toa maelezo na maagizo/
Waingie salama na kutoka hivyo hivyo/
Weka vifaa vya usalama kwa kila mtu/
Maana afya na usalama ni haki ya kila mtu/ukiwa  mwajiri ni lazima/
Utoe kifaa cha kinachofaa cha kulinda, ikiwa wafanyakazi wanaachwa wazi kwa mazingira ya kuumiza..
Ppe wanaita/ yeah!
Na ppe inayohitajika inatofautiana kulingana na kazi inayofanyika/
Kusiwe na hatari ya kitu chochote/
Iwe vifaa, wanyama, ama sumu yoyote/
Na pia.. Hakikisha usafi unaostahili/
Toa maji kwa wingi/
Na idadi ya kutosha ya vyoo nayo ya msingi/
Na pia mahali  wanapobadili nguo wafanyakazi , na mahali  wanakopumzika wafanyakazi nako ni muhimu pawe safi na sahihi/
Na kumbuka, unapowafanyia yote hayo/
Sio ruhusa kuwakata kwenye mishahara yao/

Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini

Baada ya vingi vya kumwambia/
Bosi.. Nafunga kipindi na waajiriwa/
Kwanza.. Msipende mambo ya kurahisisha/
Msianze kwanza kazi kabla ya kuhakikisha/
Uzima wa miundo mbinu hadi milango madirisha/
Vyumba vina hewa na mwanga wa kuridhisha/
Kisha vaeni vifaa vya kujilinda/
Hata kama vinachosha ila vitawakinga/
Na msione ka karaha ndogo ndogo/
Mkishatumia msiache vifaa hovyo hovyo/ kama kuna maji yanamwagika yakaushwe/
Kama kuna vumbi linazalishwa lifutwe/
Kumbuka na kuzima unapowasha umeme/
Na kama kuna nyaya zimechubuka useme/
Usisite kuripoti unapoona tatizo/
Usipuuze chochote upewapo angalizo/
(na ni hatari) kufanya kazi kupindukia/
Nchi nyingine hichi ni kinyume na sheria/
Mtu aliyechoka ni rahisi kukosea/
Haya sio maneno yangu ni tafiti zinaongea/
Usiume kisa unataka ufanyakazi bora/
Ofisi haikui kwa vifo na wafanyakazi wagonjwa/
Hadi hapo  sina kingine cha kusema/
Nimemaliza zaidi niwatakie kazi njema/

 Become A Better Singer In Only 30 Days, With Easy Video Lessons!

Written by: Adam Seleman

Lyrics © DistroKid

Lyrics Licensed & Provided by LyricFind

Discuss the Usalama Na Afya Lyrics with the community:

0 Comments

    Citation

    Use the citation below to add these lyrics to your bibliography:

    Style:MLAChicagoAPA

    "Usalama Na Afya Lyrics." Lyrics.com. STANDS4 LLC, 2024. Web. 20 May 2024. <https://www.lyrics.com/lyric-lf/11654408/Micshariki+Africa+%26+Adam+Shule+Kongwe/Usalama+Na+Afya>.

    Missing lyrics by Micshariki Africa & Adam Shule Kongwe?

    Know any other songs by Micshariki Africa & Adam Shule Kongwe? Don't keep it to yourself!

    Browse Lyrics.com

    Quiz

    Are you a music master?

    »
    "Still Into You" is a 2013 biggest hit single for which band?
    A Chairlift
    B Paramore
    C Echosmith
    D MisterWaves

    Free, no signup required:

    Add to Chrome

    Get instant explanation for any lyrics that hits you anywhere on the web!

    Free, no signup required:

    Add to Firefox

    Get instant explanation for any acronym or abbreviation that hits you anywhere on the web!

    Micshariki Africa & Adam Shule Kongwe tracks

    On Radio Right Now

    Loading...

    Powered by OnRad.io


    Think you know music? Test your MusicIQ here!